PNEUMONIA
Pneumonia: Ugonjwa Hatari Unaovamia Mapafu - Fahamu Sababu, Dalili na Tiba.
AFYAYAKO'MKONONI | Afya Yako, Uelewa Wako
Pneumonia ni ugonjwa wa mapafu unaosababishwa na maambukizi yanayopelekea uvimbe na kujazwa kwa majimaji au usaha katika vifuko vya hewa (alveoli). Hali hii huathiri uwezo wa mapafu kupitisha hewa safi na kuleta upungufu wa oksijeni mwilini.
Sababu Zinazosababisha Pneumonia
Pneumonia inaweza kusababishwa na:
@1. Bakteria (kama Streptococcus pneumoniae)
@2. Virusi (kama virusi vya mafua na COVID-19)
@3. Fangasi (hasa kwa watu wenye kinga hafifu)
Aina za Pneumonia
1. Pneumonia ya Jamii (Community-acquired): Inatokea kwa watu walioko nje ya hospitali.
2. Pneumonia ya Hospitali (Hospital-acquired): Huibuka baada ya siku 2 au zaidi tangu kulazwa.
3. Pneumonia ya Ventilator (VAP): Inatokea kwa wagonjwa waliowekwa kwenye mashine ya kupumulia.
4. Aspiration Pneumonia: Husababishwa na kuvuta mate au chakula kuingia kwenye mapafu.
Watu Walio katika Hatari Zaidi
1. Wavutaji wa sigara
2. Watu waliopata maambukizi ya awali
3. Wagonjwa waliopasuliwa
4. Wenye magonjwa sugu ya mapafu
5.Watu wenye kinga dhaifu (kama wenye VVU)
Dalili za Pneumonia
1. Kikohozi chenye makohozi ya usaha
2. Homa kali
3. Kupumua kwa shida au haraka
4. Mapigo ya moyo kwenda kasi
5. Maumivu ya kifua
6. Kupungua kwa kiwango cha oksijeni mwilini
7. Kuongezeka kwa seli nyeupe (WBC) na CRP
Matibabu ya Pneumonia
Antibiotiki kwa maambukizi ya bakteria
Dawa za virusi kwa pneumonia ya virusi
Dawa za fangasi kwa maambukizi ya fangasi
Oksijeni kusaidia upumuaji
Maji ya kutosha (kupitia dripu au kunywa)
Dawa za kushusha homa na maumivu
Kifaa cha kusaidia kupumua (ventilator) kwa hali mbaya
Physiotherapy ya kifua kusaidia utoaji wa makohozi.
Hitimisho
Pneumonia ni ugonjwa unaoweza kuepukika na kutibika iwapo utatambuliwa mapema na kutibiwa ipasavyo. Elimu ya afya, chanjo, na ufuatiliaji wa dalili ni hatua muhimu za kinga.
Tembelea blog yetu kila wiki kwa maarifa zaidi ya afya moja kwa moja kutoka kwa simu yako — AfyaYako'Mkononi.
Comments
Post a Comment